Chatanda: Bandari haijauzwa, ni maneno ya wapotoshaji

0
134

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Mary Chatanda amesema bandari ya Dar es Salaam haijauzwa kama wanavyosema baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na Taifa.

“Naomba kuwahakikishia suala hili lipo vizuri wala bandari haijauzwa kama wanavyosema baadhi kuwa bandari imeuzwa. Hayo ni maneno ya wapotoshaji na kipindi hiki mtasikia mengi. Rais Samia hawezi kuuza Bandari na wala hajaingia mkataba wa huo wanaosema wa miaka 100, bado wapo kwenye mazungumzo”. Amesema Chatanda

Alikuwa akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha ziara ya viongozi wa UWT Taifa mkoani Njombe.

“Hata shukurani hakuna, mikataba ya huko nyuma ilikuwa inasainiwa tu juu kwa juu lakini Rais Samia muwazi ameamua kupeleka mkataba mbele ya Bunge ujadiliwe, imekuwa nongwa?”.

“Bandari hii walipewa Wawekezaji na mapato yalikuwa yanaingia ni kidogo. Sasa tuendelee na mtu anatupa Trilioni 7?… Kama tumepata mwekezaji anataka kutupa Trilioni 26 bora”.
Amesema Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa, Mary Chatanda