MWENDOKASI KUIFUNGUA KARIAKOO SAA 24

0
141

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema uendelezaji wa miundombinu hususani ile ya miradi ya barabara na mabasi Yaendayo Haraka mkoani Dar es Salaam utachangia kufungua masoko likiiwemo Soko Kuu la Kariakoo kufanya kazi saa 24.

Chalamila ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalum kupitia TBC Aridhio.

“Utaungana nami kwamba miundomhinu tu hii ambayo inatengenezwa sasa ni miundonbinu ya gharama kubwa sana kwenye haya mabasi ya mwendokasi. Kuna Bilioni karibu 231.7, kuna Bilioni 217 lakini zaidi utaona juzi tena tumesaini mkataba kwa ajili ya barabara hii inayotoka mwenge kuelekea kule Tegeta”.

“Sasa nani atapanda haya mabasi?. Ndio maana tukasema ni vizuri tukawaza sasa kufanya biashara hizi za mabasi masaa 24 lakini watu hao wanaelekea wapi?….. ni vizuri tuka connect [unganisha] abiria sasa na masoko yetu ya Kariakoo ili kule Kariakoo watu watakapofika sasa biashara nako ziwe saa 24.“ Amesema Chalamila