HALMASHAURI, MANISPAA KUANZISHA DAMPO LAKE

0
129

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema moja ya njia za kutoa suluhu ya changamoto ya uchafuzi wa mazingiza kutokana na dampo kujaa taka ni kuzielekeza kila halmashauri na manispaa kuwa na dampo lake na sio kuchangia dampo kama ilivyo sasa.

Chalamila ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum kupitia TBC Aridhio.

Chalamila amesema
“Lazima kila halmashauri na kila manispaa cha kwanza iwe na dampo lake na sio kwenda kumwaga tena kule Pugu ambako wanachangiana uchafu lakini pasipo kuwa na sustainability [uhimilivu] ambayo inaweza kuwa ni safi kwa ustawi wa mji wetu….”

“Kwa hiyo jambo la kwanza nimekwisha elekeza lazima kila manispaa ianzishe mchakato wa kukusanya takataka lakini kuweza pia kuzi process [kuzichakata], tunataka tubadilishe takataka ‘ waste’ ziende kwenye energy [nishati] ……waste [taka] ziwe pesa au waste [taka] ziwe ajira”

“….na kwa mantiki hiyo ni kwamba tukishafikia hiyo hatua ya takataka kuzibadili kuwa fedha …. takataka kuzibadili kuwa nishati ….kuwa ajira maana yake ni kwamba mji huu wote takataka zitapotea…..,
sasa tumekwisha anza kufanya mchakato wa kuhakikisha kwamba tunakuwa na wawekezaji lakini pia tutatumia bajeti za ndani kuhakikisha kwamba tu funga mitambo mikubwa ya uchakataji wa takataka ambazo zitaweza kutusaidia kuzalisha nishati au mbolea kwenye taka zilizooza…..lakini na kutenganisha zile takataka ambazo haziozi.”