Vikosi vya serikali nchini Sudan vimelazimika kutumia mabomu ya machozi pamoja na risasi za mpira kutawanya waandamanaji katika mitaa mbalimbali ya mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum, kushinikiza kujiuzulu kwa Rais Omar Al-Bashir.
Waandamanaji hao walifika hadi katika Makao Makuu ya Jeshi la Sudan yaliyopo kwenye mji huo wa Khartoum ambapo walikua wakiwataka askari kuungana nao katika kampeni yao ya kumuondoa madarakani Rais Al-Bashir.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa katika Makao Makuu hayo ya Jeshi la Sudan askari walikua wakiwazuia waandamanaji hao wasipate hatari yoyote na wengine walikua wakiwazuia askari wenzao waliokua wakirusha mabomu ya machozi pamoja na risasi za mpira wasiwadhuru waandamanaji.
Habari zaidi kutoka nchini Sudan zinasema kuwa baadhi ya waandamanaji walipatiwa malazi ndani ya Makao Makuu ya Jeshi la Wana Maji la nchini Sudan.