Serikali yasisitiza kupiga marufuku mifuko ya plastiki

0
298

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amesema kuwa serikali ina mpango wa kusitisha matumizi pamoja na uzalishaji wa mifuko ya plastiki ili kuzuia uharibifu wa mazingira.

Waziri Makamba ameliambia Bunge jijini Dodoma  kuwa kuna uwezekano hatua hiyo ikafikia utekelezaji Julai Mosi mwaka huu baada ya kukamilika kwa taratibu mbalimbali.

Amesema kuwa tayari ameishaelekezwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutekeleza jambo hilo kwa kushirikisha wadau mbalimbali na kinachoendelea hivi sasa ni kukutana na wadau hao, lengo likiwa ni kufikia makubaliano.