Amzalisha mkwewe miaka 22 nyuma

0
234

Mwanamama mmoja mkunga raia wa Marekani hivi karibuni amegundua kuwa miaka 22 iliyopita alimshika mkwewe mikononi mwake.

Wakiwa wanaangalia picha zao za utoto za Kelsey Poll mumewe Tyler West alishtuka baada ya kuona sura anayoifahamu.

Alikuwa ni mama yake mzazi Mary Ann West akiwa amembeba mkewe Kelsey.

“Ilitulishangaza. Ilikuwa kama jambo lililokusudiwa kutokea. Kuna uwezekano gani kwamba watoto hawa wawili wangekutana waoane na kuanzisha familia yao?”Amesema mama mkwe.

Mary Ann anasema hawezi kusahau siku ambayo Stacy Poll alienda kujifungua kwani ujauzito wake ulikuwa na changamoto kadhaa na Stacy alikuwa na wasiwasi hali iliyomfanya ampe baadhi ya ushauri wa namna bora ya kulea mwanae huyo.

Kelsey Poll West ni mtoto wa tatu wa Stacy Tyler akiwa ni mtoto wa tatu wa Mary Ann.