Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeanza mazungumzo na Shirika la Sayansi na Teknolojia la Anga la China (CASC) kwa ajili ya kushirikiana katika Teknolojia ya Anga za Juu na Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Mazungumzo hayo yamefanyika kwa njia ya video na kushirikisha uongozi wa wizara akiwemo Waziri Nape Nnauye , Katibu Mkuu Mohammed Khamis Abdulla, Naibu Katibu Mkuu Selestine Kakele pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Tume ya TEHAMA na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Mazungumzo hayo ni hatua nyingine ya Serikali ya kuwa na mikakati endelevu ya kujenga na kukuza uchumi wa kidijitali wenye kuleta tija na maisha bora kwa kila Mtanzania kupitia TEHAMA.
#TZDigitalTrasformation #TanzaniayaKidijitali #KaziIendelee