Wananchi Mtama sasa kupikia gesi

0
211

Waziri Wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi amegawa mitungi ya gesi 250 ambayo kati hiyo 85 amewapatia Wanachama wa kikundi cha Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) halmashauri ya Mtama.

Akizungumza na Wananchi wa jimbo la Mtama Waziri Nape amesema, mitungi mingine 200 ya gesi aliyopewa na Waziri wa Nishati January Makamba itapelekwa katika jimbo hilo na itatolewa kwa utaratibu ili Wananchi wote wa Mtama waweze kutumia nishati bora katika kupikia.

Baadhi ya Wananchi wa Mtama wamemshukuru Waziri Nape kwa kuwaondoa katika matumizi ya kuni na mkaa na kusema kuwa kwa sasa wanakwenda kutumia gesi.