Nakufahamisha tu! Miaka 25 ya NMB ni leo

0
1046

Benki ya NMB leo inatimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake, ikiwa imeanzishwa kwa Sheria ya Bunge ya ‘The National Microfinance Bank incorporation Act ya mwaka 1997 baada ya kugawanywa iliyokuwa benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

Kwa historia safari ya mafanikio ya benki ya NMB ilianza kama benki iliyokuwa ikitoa huduma ya malipo ya mishahara na pensheni kwa Watumishi wa umma, kufungua akaunti za akiba na kutoa mikopo ya kiwango kidogo.

Benki ya NMB ilianza ikiwa na matawi madogo ya kibenki 97, kwa kipindi hicho matawi hayo yalikuwa ndio njia pekee ya kuwahudumia wateja wake kwa wepesi kwani haikuwa na mashine za kutolea pesa (ATMs mashine) wala mawakala wa kibenki.

Mwaka 2005 benki ya NMB ilibinafsishwa na hapo ndipo safari yake ya mafanikio iliposhika kasi na kuendeleza maono ya kuijenga NMB ya sasa.

Kufahamu mengi zaidi kuhusu safari ya mafanikio ya benki ya NMB usikose kufuatilia matangazo yatakayokufikia hivi punde kupitia Televisheni kwa chaneli ya TBC1 na mitandao yetu ya kijamii kwa anwani ya TBCOnline.