Miradi ya maendeleo Mwanza

0
194


Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Amos Makalla ametaja miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa mkoani humo na kuwanufaisha wananchi.

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Bujora uliogharimu shilingi Bilioni 1.4 na ujenzi wa jengo la utawala katika halmashauri ya wilaya ya Magu kwa gharama ya shilingi Bilioni 5.4.

Miradi mingine ni ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana Bugashi inayotarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu kwa gharama ya shilingi Bilioni 3 na ukarabati wa hospitali, vifaa na vituo vya afya Magu kwa shilingi Bilioni 1.1.

Makalla ameongeza kuwa jumla ya shilingi Bilioni 94 zimetumika kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya elfu mbili kwa mkoa mzima wa Mwanza.

Makalla ameyasema hayo katika Tamasha la Utamaduni Bulabo ambapo pia ameishukuru Serikali kwa kupeleka fedha nyingi mkoani Mwanza kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.