Kiungo Mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Junior atavaa jezi namba 7 kuanzia msimu ujao, ambayo awali imevaliwa na Eden Hazard na Cristiano Ronaldo.
Kabla ya kubadili namba, Vini amevaa jezi namba 20 kwa miaka yake minne aliyokaa Bernabeu.
Naye kinda wa Brazili, Rodyrigo, atavaa jezi namba 11, ambayo ilikuwa inavaliwa na Marco Asensio, badala ya 21 aliyokuwa akivaa hapo awali.