Uteuzi NMB, NDC, MOI na NM – AIST

0
181

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Omar Issa kuwa Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).

Issa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na anachukua nafasi ya Dkt.Gharib Bilal, Makamu wa Rais Mstaafu ambaye amemaliza muda wake.

Profesa Abel Makubi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI) na anachukua nafasi ya Dkt. Respicious Boniface ambaye amemaliza muda wake.

Rais Samia pia amemteua Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee kuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) na kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na anachukua nafasi ya Balozi Marten Lumbanga aliyemaliza muda wake.

Dkt. Edwin Mhede yeye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB Plc kwa kipindi cha pili.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza Juni 06, 2023.