Mohamed Raza afariki dunia

0
189

Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar na Mwanasiasa mkongwe ambaye aliwahi kuwa Mwakilishi wa jimbo la Uzini mkoa wa Kusini Unguja, Mohamed Raza amefariki dunia leo mkoani Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mmoja wa Wanafamilia aitwaye Mohammed Ibrahim Raza.