Bunge limepitisha azimio la kutofanya kazi na CAG Profesa Assad, huku Mbunge wa kawe Halima Mdee akisimamishwa mikutano miwili

0
509

Bunge limepitisha azimio la kutofanya kazi wala kushirikiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali -CAG Profesa MUSSA ASSAD kwa madai ya kulidhalilisha Bunge wakati akihojiwa na chombo kimoja cha kimataifa.

Uamuzi huo wa bunge umetolewa bungeni mjini DODOMA baada ya mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya haki maadili na madaraka ya bunge EMMANUEL MWAKASAKA kutoa hoja bungeni ya kamati kuhusu azimio la kufanya kazi na CAG.