Wizara ya Mifugo na SUA wasaini makubaliano

0
192

Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) wamesaini makubaliano ya kushirikiana katika kuwawezesha vijana kujiajiri pamoja na kuinua sekta za mifugo na Uvuvi nchini.

Akizungumza mkoani Morogoro mara baada ya hafla ya utiaji saini makubaliano hayo iliyofanyika SUA, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega amesema, tukio hilo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wakulima (Nanenane) mkoani Mbeya Agosti 8, 2022.