Wizara ya Michezo, BMT kununua tiketi 10,000 mechi ya Yanga

0
185

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) zimeahidi kununua tikieti 10,000 kwa ajili ya mashabiki kushuhudia mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga SC na USM Alger ya Algeria.

Katibu Mtendaji wa BMT, Neema Msita amesema wameunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye hivi karibuni ameahidi kununua tiketi 5,000 kwa ajili mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Jumapili ya wiki hii

Wiki iliyopita Rais Samia alitangaza kuongeza dau la magoli kwenye fainali kufikia TZS milioni 20 kwa kila goli la ushindi pamoja na kutoa ndege ya kuipeleka Yanga nchini Algeria na kuirejesha nchini.