Rais Samia ateua Majaji sita Mahakama ya Rufaa

0
313

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufaa sita, uteuzi ambao umeanza Aprili 28 mwaka huu.

Kwanza, amemteua Jaji Zainab Goronya Muruke kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ambapo kabla ya uteuzi huo, alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi cha Mashauri ya Ndoa, Talaka na Mirathi – Temeke, Dar es Salaam.

Pili, amemteua Jaji Dkt. Benhajj Shaaban Masoud kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. ambaye alikuwa Mkuu wa Shule ya Sheria Tanzania.

Tatu, amemteua Jaji Amour Said Khamis kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora.

Nne, amemteua Jaji Leila Edith Mgonya kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Masijala Kuu Dar es Salaam.

Tano, amemteua Jaji Gerson John Mdemu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Sita, amemteua Jaji Agnes Zephania Mgeyekwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi.

Taarifa kutoka Ikulu imeeleza kuwa wateule hao wataapishwa kwa tarehe ambayo itapangwa baadaye.