City na Madrid ni mechi ya kisasi na rekodi

0
380

Kivumbi kesho katika dimba la Etihad jijini Manchester ambapo Manchester City itawakaribisha wababe wa UEFA, Real Madrid katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilikwenda sare ya 1-1 katika dimba la Bernabeu.

Wakati City akitaka ushindi ili kuiweka hai ndoto ya kushinda makombe matatu msimu huu na kulipiza kisasi kwa kutolewa kwenye mashindano hayo na Madrid mwaka jana, miamba hiyo ya Hispania yenyewe inataka ushindi ili kujipooza na machungu ya kuukosa ubingwa wa La Liga.

City tayari imeukaribia ubingwa wa Ligi Kuu ya England, ikiwa sasa inahitaji alama tatu tu katika mechi tatu ilizonazo na tayari imetinga fainali ya Kombe la FA ambapo itakutana na Manchester United mwezi Juni mwaka huu.

Madrid wao wanawinda kombe la pili baada ya kushinda Copa del Rey mapema Mei mwaka huu ikiifunga Osasuna.

Ni mechi ya kisasi, ni mechi ya wababe ni nusu fainali kama fainali, mmoja atafurahi na mmoja atalia, muda utaamua.