Jela miaka 20 kwa kulaghai wazungu

0
187

Mrembo kutoka Ghana Mona Faiz Montrage maarufu Hajia 4Real, amefukuzwa nchini Uingereza na kupelekwa Marekani baada ya kushtakiwa kwa kashfa ya kurubuni kimapenzi Dola Milioni mbili za Kimarekani.

Tayari Hajia amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela nchini Marekani.

Waendesha mashtaka wa Serikali ya Marekani wamesema Hajia ametiwa hatiani kwa kulaghai fedha hizo kutoka kwa wazee wa kizungu wenye upweke nchini humo ambapo aliwaahidi mapenzi.

Kwa miaka mingi, mwanadada huyo amekuwa akionesha magari na majumba yake ya kifahari mitandaoni na kuwafanya mashabiki wake kumpongeze mara kadhaa kwa mafanikio yake.