Mbowe : Membe alikuwa mwanasiasa mbobezi Kitaifa na Kimataifa

0
241

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe amesema licha ya kuwa katika vyama tofauti na Bernard Membe, kuna mambo waliweza kushirikiana katika ujenzi wa Taifa.

Mbowe amesema hayo alipofika nyumbani kwa marehemu Membe Mikocheni, Dar es Salaam kutoa pole kwa Wanafamilia kufuatia kuondokewa na mpendwa wao.

Mbowe amesema Membe alikuwa mwanasisa mbobezi Kitaifa na Kimataifa, hivyo kifo chake ni pigo kwa Taifa.

“Membe alikuwa ni mtu aliyejitambua na aliweza kufikiwa na kila mtu, hata pale tulipotofautiana katika vyama vyetu bado aliweza kuheshimu haki ya kila mtu”.Amesema Mbowe.

Bernard Membe aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, alifariki dunia hapo jana katika hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam.