Rais afanya uteuzi mfuko wa Mafuta na Gesi

0
195

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mussa Mohamed Makame ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri na Uwekezaji ya Mfuko wa Mafuta na Gesi (Portfolio Investment Advisory Board).

Aidha, Rais Samia amewateua wajumbe wa Bodi hiyo ambao ni Dkt. Suleiman Missango (Meneja Msaidizi Kurugenzi ya
Utafiti na Sera, Benki Kuu ya Tanzania),
Safiel Msovu (Afisa Fedha Mwandamizi, Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania), Shogholo Msangi (Mkurugenzi wa Kampuni ya Express
Microfinance Company Ltd) na
Mwanaidi Manda( aliyewahi kuwa Mhasibu Mkuu wa
Serikali).

Uteuzi huo umeanza Mei 11, 2023.