Dementia inayofahamika sana kama
shida ya akili sio ugonjwa, bali ni hali inayosababisha mtu kukosa uwezo wa kutunza kumbukumbu, kufikiri na kushindwa kufanya maamuzi yanayohusu shughuli zake za kila siku.
Hali hii inawapata zaidi wazee kutokana na kuwa na umri mkubwa, japo si kila mzee hupatwa na hali hiyo.
Miongoni mwa vyanzo vya tatizo hilo ni kuharibika kwa seli za ubongo na kupoteza mawasiliano kwa sababu ya msongo wa mawazo, upweke, shinikizo la damu na uvutaji wa sigara.
Watu wenye
Dementia ama
shida ya akili wanaweza kushindwa kutambua kabisa familia zao na rafiki zao.
Jamii inayoishi na watu wa hali hiyo wanashauriwa kuwajali na kuwa karibu nao, kwa kuwasaidia waimarike kiafya pamoja na kufanya kazi za kijamii.