Adai pesa za picha za harusi baada ya talaka

0
319

Aliyekuwa mteja wa mpiga picha mashuhuri nchini Afrika Kusini Lance Romeo mwaka 2019, amedai arejeshewe angalau asilimia 70 ya pesa aliyolipia picha za harusi yake kwani ametalikiana na mumewe na hazihitaji tena picha hizo.

Akiwa mwenye ghadhabu Mwanamama huyo alimtafuta Romeo na kumkumbusha kuwa alipiga picha za harusi yake huko Durban na sasa hazihitaji picha hizo hivyo angeomba arejeshewe fedha zake la sivyo atamhusisha mwanasheria wake.

“Ulizifanyia kazi nzuri sana lakini kwa sasa ni sawa na bure kwa vile tumeachana, nitahitaji mrejesho wa kiasi tulichokulipa kwa sababu hatuzihitaji tena,” Ameandika mwanamama huyo

“Tayari nimekupa huduma na picha,” amejibu Romeo

“Siwezi kukurejeshea pesa kwa sababu siwezi kurudisha nyuma,” ameendelea kujibu Romeo na kuongeza kuwa “Ningependa tuzungumze kikazi na kukuhakikishia tu kwamba HAUTAREJESHEWA pesa. Inasikitisha kwamba unataka kurejeshewa pesa miaka 4 baadaye, kwa bahati mbaya ni aibu kwa upande wako.”

Baada ya vitisho kushindwa kuleta muafaka, mwanamama huyo aliomba kukutana uso kwa uso na Romeo ambaye amekataa.