Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tabia Maulid Mwita amesema, mchakato wa marekebisho ya Sheria ya Habari Zanzibar umefika asilimia 80.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika Kitaifa jijini Zanzibar Waziri Tabia amesema, Sheria hiyo itajumuisha mawazo ya Waandishi wa habari ambayo tayari yamekusanywa.
Ameongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendela kuboresha mazingira ya upashanaji habari, ili kutoa haki ya uhuru wa habari.