Nape ataka ajenda mahususi kutokomeza Malaria

0
216

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini, kampuni za simu na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa na ajenda mahususi katika vita dhidi ya Malaria, ili kuutokomeza ugonjwa huo.

Waziri Nape amayasema hayo wakati wa maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika mkoani Dar es Salaam.

“Naagiza kuwa vyombo vyote nchini vinatakiwa kuwa na mpango wa kutokomeza malaria, Niombe Pia kila anayetumia mitandao ya kijamii anakuwa na ajenda ya mapambano dhidi ya Malaria na makampuni yote ya simu yahakikishe nayo yanakuwa na mpango wa kutokomeza Malaria nchini.” Amesisitiza waziri Nape

Siku ya Malaria Duniani huadhimishwa Aprili 25 ya kila mwaka na kauli mbiu ya kitaifa ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni ‘Wakati wa kutokomeza Malaria ni sasa badilika, wekeza, Tekeleza – Ziro Malaria inaanza na Mimi’.