Marekani kuisaidia Tanzania kutokomeza Malaria

0
167

Balozi wa Marekani nchini Michael Battle ameahidi kuwa Serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania na taasisi nyingine, ili kufanikisha mapambano dhidi ya Maralia.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Malaria Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam Balozi Battle amesema, Marekani itaendelea kushiriki katika mapambano hayo hadi Tanzania itakapofikia asilimia sifuri ya maambukizi ya Malaria.

Kwa mujibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti na Kutokomeza Malaria, vifo vitokanavyo na Malaria vimepungua kwa asilimia 76 kutoka vifo 6,311 mwaka 2015 hadi vifo 1,502 mwaka 2022 huku waliothibitishwa kuugua Malaria wakipungua kutoka watu milioni 7.7 mwaka 2015 hadi watu milioni 3.5 mwaka 2022.

Nayo maambukizi ya Malaria nchini yamepungua ambapo mwaka 2008 takwimu zilionesha kuwa asilimia 18.1 walikuwa na Malaria ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2022 ambapo kiwango kilikuwa asilimia 8.1.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwa mwqka huu ni ‘Wakati wa Kutokomeza Malaria ni Sasa Badilika, Wekeza, Tekeleza – Ziro Malaria inaanza na Mimi’.