TANESCO yawadai wateja Bilioni 244

0
192

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawadai shilingi Bilioni 244 wateja wake mbalimbali, wakiwemo wateja wa umma na wateja binafsi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Tawhida Galos aliyehoji kuna mpango gani wa kukusanya madeni ya TANESCO katika taasisi kubwa ili shirika hilo liweze kujiendesha.

Byabato ameongeza kuwa ili kuzuia ukuaji na kuwezesha ukusanyaji wa madeni, TANESCO wameweka mita za LUKU kuhamasisha na kufuatilia madeni na inapobidi kukata huduma ya umeme kwa wateja wenye deni kubwa na sugu ili liweze kulipwa.