Elon Musk apata harasa

0
281

Wakati macho yakielekezwa kwenye kurasa za watu mashuhuri kwenye mtandao wa Twitter wanaoondolewa alama ya bluu ‘Blue tick’ na wengine kujitoa kwenye mtandao huo unaomilikiwa na Bilionea Elon Musk, Bilionea huyo amekumbwa na mkasa mkubwa zaidi.

Mkasa huo ni kulipuka angani kwa roketi ya SpaceX Starship inayomilikiwa na Elon Musk, ambayo imelipuka dakika chache baada ya kurushwa kwa majaribio.

Roketi ya SpaceX Starship inatajwa kuwa ni kubwa zaidi kuliko zote zilizowahi kutengenezwa.

Pamoja na kupata hasara hiyo, Musk amesema wanajipanga upya kama kampuni na watafanya jaribio lingine ndani ya miezi michache ijayo.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo ya
kulipuka angani kwa roketi ya SpaceX Starship.