Ku-bet pesa za mradi ni uhujumu uchumi

0
196

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wawekezaji wanaotumia pesa za miradi kama fursa za kujikuza kiuchumi kuacha mara moja kufanya hivyo.

“Tuna mtindo ndugu zangu Wawekezaji, tunachukua miradi na kwenda kuweka ‘deposit’ zetu kwenye ‘stock exchange’, tunagenerate fedha kwanza alafu ndio turudi kuwekeza bila kujali kwamba huu ni uhujumu uchumi kwa nchi yetu.” Amesema Rais Samia

Alikuwa akizungumza Ikulu Chamwino mkoani Dodoma katika hafla ya utiaji saini mikataba ya makubaliano kati ya Serikali na kampuni za madini kutoka Australia.