Macho na masikio ya mashabiki wa mbio leo yapo nchini Marekani katika mashindano ya mbio ndefu ya Boston (Boston Marathon) mwaka 2023 ambapo kwa Tanzania inawakilishwa na Gabriel Geay.
Geay atakuwa akichuana na wanaridha mahiri kutoka Kenya, Eliud Kipchoge na Evans Chebet na Herpasa Negasa wa Ethiopia.
Mshindi wa mbio hizo zinazofanyika kwa mara ya 127 atakwenda nyumbani na taji la ubingwa lakini pia kitita kizuri cha fedha ambacho kitahusisha TZS bilioni 2.06 ambazo zitagawiwa kwa washindi wote.
Mshindi wa mbio hizo kwa nafasi ya kwanza ataweka kibindoni TZS milioni 352.
Zaidi ya wanamichezo 30,000 kutoka kutoka katika nchi 100 duniani wanatarajiwa kushiriki.