Katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24, Shirika la Masoko ya Kariakoo limeomba kuidhinishiwa shilingi bilioni 1.68 kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Kati ya fedha hizo, shilingi milioni 747.54 ni kwa ajili ya mishahara na shilingi milioni 938.44 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.
Pia shirika litaendelea na ujenzi wa soko jipya na ukarabati wa soko lililoungua unaotarajiwa kukamilika Oktoba, 2023.
Aidha, shirika litaandaa Mpango wa Uwekezaji katika maeneo inayomiliki yaliyopo Mbezi Beach Makonde katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na Tabata Bima katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.