Serikali yaomba radhi kufuatia sakata la “Prison Break”

0
376

Kufuatia kurudishwa kwa Thabo Bester nchini Afrika Kusini baada ya kujitengenezea kifo chake, Serikali ya Afrika Kusini imewaomba radhi wananchi pamoja na familia za waathirika wa majanga mikononi mwa Bester kufuatia kutoroka kwa mtuhumiwa huyo jela na kuwa huru kwa kipindi kirefu.

Bester amefikishwa kizimbani leo kujibu shitaka jipya la kutoroka gerezani alipokuwa akitumikia kifungo cha maisha. Mpenzi wake, Nandipha Magudumana ambaye ndiye msaada mkuu wa kutoroka kwa Bester gerezani naye anashikiliwa kwa mauaji na atapanda kizimbani hivi karibuni.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo imethibitisha kuwa, japo Bester ni raia wa Afrika Kusini hana rekodi zozote za uhalali wake wa kuwa raia wa nchi hiyo ikiwemo ni pamoja na kukosa kitambulisho cha taifa au pasipoti.

Maswali yanabaki kuwa kwanini Nandipha ambaye ni daktari, mke, na mama wa watoto wawili aliamua kumtorosha Bester na kukimbia naye. Habari zaidi tutakuletea hapa hapa TBCOnline.