Baiskeli ya boksi, utainunua?

0
313

Mhandisi mmoja maarufu katika chaneli ya YouTube ya The Q ametengeneza baiskeli yenye matairi ya kiboksi, tofauti na ilivyo sasa kwa matairi kuwa duara na baiskeli hiyo inafanya kazi vizuri kabisa.

Si wazo jipya kuwa na matairi ya mraba, Mythbusters waliwahi kutengeneza gari lenye matairi hayo na matokeo yake hayakuwa mazuri, ila baiskeli hii inazunguka kwa haraka kama ile yenye matairi ya duara.