Kocha wa Al-Nassr afukuzwa kisa Ronaldo

0
544
Soccer Football - Al Nassr unveil new signing Cristiano Ronaldo - Mrsool Park, Riyadh, Saudi Arabia - January 3, 2023 Al Nassr coach Rudi Garcia and new signing Cristiano Ronaldo during the press conference REUTERS/Ahmed Yosri

Kocha wa Al-Nassr ya Saudi Arabia, Rudi Garcia amefukuzwa kazi baada ya kudaiwa kuwepo hali ya kutoelewana kati yake na Cristiano Ronaldo.

Imeelezwa kuwa mgogoro kati ya wawili hao umetokana na timu kutokufanya vizuri huku Ronaldo akiona kuwa Gracia hafanyi vya kutosha kuisaidia timu hiyo.

Suluhu katika mchezo dhidi ya Al-Fayha uliifanya Al-Nassr kuwa na alama tatu nyuma ya vinara wa ligi Al-Ittihad, hali inayoripotiwa kutomfurahisha Ronaldo ambaye anapingana na mbinu za kiufundi za kocha huyo.

Gracia ambaye amewahi kuifundisha Roma na Lyon, alikabidhiwa wadhifa huo mwezi Juni 2022.