KimataifaCHADEMA WAICHAMBUA RIPOTI YA CAGBy Adrina mariki - April 10, 20230519ShareFacebookTwitterWhatsAppLinkedin MUHIMU NI HATUA ZILIZOCHUKULIWA”Kwa kuwa ripoti hizi zilianza kuelezwa maudhui yake na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Rais tarehe 29 mwezi Machi na kuwekwa hadharani toka tarehe 6 mwezi Aprili, kitu cha muhimu kwa Taifa kwa sasa ni kutafakari kwa pamoja sio tu uchambuzi wa maudhui bali zaidi uchambuzi wa hatua zilizochukuliwa na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.” John Mnyika,Katibu Mkuu CHADEMAHATUA ZILIZOCHUKULIWA TRC HAZITOSHI“Kitendo cha kuvunja Bodi peke yake sio hatua toshelevu ikilinganishwa na kiwango cha ufisadi na hasara na ubadhilifu ambao kama Taifa tumepata kutokana na jambo hili. Na ukiondoa suala la kutafutwa mzabuni wa gharama ya juu, ufisadi wa Shirika la Reli ulihusu vilevile ununuzi wa localmotives na mabehewa kwa mkataba mbovu bila kuwepo kwa dhamana, na Serikali kupata hasara nyingine ya Bilioni 13.7. Kwa msingi huu hatua ambazo zimechukuliwa na Ikulu juu ya shirika la Reli bado hazijitoshelezi.”John MnyikaKatibu Mkuu CHADEMASERIKALI IWEKE BAYANA MADAI YOTE“Nitoe wito kwa Mheshimiwa Rais na Serikali kuchukua hatua sio tu hiyo ya Mtendaji Mkuu [ATCL], bali Serikali iweke bayana madai yote ya ufisadi na hasara ambayo Taifa limepata kwenye ununuzi wa ndege za Serikali na kwenye uendeshaji wa shirika la ATCL na kuchukua hatua kwa mawaziri waliohusika na mchakato huu na makatibu wakuu waliohusika na mchakato huu. Hatua kamili ambazo zitaonesha kweli Serikali imedhamiria kufungua ukurasa mpya wa uwajibikaji ndani ya Serikali.”John Mnyika,Katibu Mkuu CHADEMAWATUHUMIWA WA UFISADI BADO WAPO SERIKALINI“Mapendekezo ya CAG yalikuwa 6,947 yaliyofanyiwa kazi ni 2,506 peke yake sawa na asilimia 36 peke yake. Mapendekezo ya PAC kati ya 272 yamefanyiwa kazi 35 peke yake, watuhumiwa wa ufisadi wa ripoti ya mwaka 2020/2021 bado wapo Serikalini, bado wapo barabarani fedha za umma hazijarudi.Kama ripoti ya mwaka jana haijafanyiwa kazi nini kitufanye tuamini kwamba ripoti ya mwaka huu itafanyiwa kazi?”. John Mnyika,Katibu Mkuu CHADEMAIMEKUWAJE?, BUNGE LITUELEZE“lakini tukiiacha hii ripoti ya 2021/2022 kuna ripoti ya 2020/2021. Hii ripoti imeshapitia utaratibu wote sasa bunge chini ya Spika Tulia litueleze hivi imekuwaje ripoti ambayo iliwekwa bungeni mwaka jana ikapelekwa kwenye kamati, Serikali ikaandaa hiyo ripoti jumuishi ikapelekwa bungeni, hivi imekuwaje chini ya Spika mapendekezo yaliyotekelezwa ni 2,500 peke yake kati ya 6,947?.Tukisema kwamba bunge hili linalinda na kulea ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma tutakuwa tumekosea?”.John Mnyika,Katibu Mkuu CHADEMA