Wakristo washerekea sikukuu ya Pasaka

0
193

Waumini wa dini ya Kikristo, leo wanaungana na wenzao katika Mataifa mbalimbali duniani kusherekea Sikukuu ya Pasaka ikiwa ni Kufufuka kwa Yesu Kristo.

Sikukuu ya Pasaka inasherekewa baada ya kukamilika kwa Mfungo wa Kwaresma, ambapo baadhi ya Waumini ya dini ya Kikristo wamekuwa katika mfungo huo kwa siku 40.

Ibada ya Pasaka Kitaifa inafanyika asubuhi hii katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu Francisco Xavery Jimbo la Tunduru – Masasi lililopo mkoani Ruvuma.