Ujumbe wa Ibada ya Ijumaa Kuu ‘TUISHI KWA AMANI’

0
210

Ujumbe wa Askofu Raphael Haule wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma katika Ibada ya Ijumaa Kuu Kitaifa kwenye Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi Kiuma, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.

– Kuishi kwa amani
– Kupendana
– Kushirikiana
– Kusaidiana
– Kusameheana
– Kuendelea kutangaza neno la Mungu

“Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu wetu aliyetupa afya na uzima tele, siku hii ni muhimu kwa Wakristo wote duniani tunapokumbuka mateso ya Mwokozi wetu Yesu Kristo anapobeba dhambi ya Mwanadamu anazikwa nayo kisha akafufuka ili kuleta ukombozi kwa ulimwengu mzima, maana yake Wakristo wote wanapaswa kuishi kwa amani, kupendana, kushirikiana, kusaidiana, kusameheana na kuendelea kutangaza neno la Mungu”. amesema Askofu Haule

Pia amesisitiza udhibiti wa unywaji pombe ili kupunguza athari ndani ya familia.

Ujumbe muhimu katika Ibada ya Ijumaa Kuu ni Utunzaji wa Mazingira.

“Kanisa lina wajibu wa kuwakumbusha Waumini wake kutunza mazingira kama Mungu alivyoagiza, sisi tunaendelea kuhimiza wajibu wa kutunza mazingira ni wa kila mtu“. amesisitiza Askofu Raphael Haule

#IjumaaKuuKitaifa2023