Faini trilioni 20.8 kwa kusababisha saratani

0
201

Kampuni ya Johnson & Johnson imekiri kutakiwa kulipa Dola Bilioni 8.9 za Kimarekani ambazo ni sawa na shilingi Trilioni 20.8 za Tanzania ndani ya kipindi cha miaka 25, kama suluhisho kwa madai ya bidhaa yake ya poda kusababisha Saratani kwa watumiaji.

Kampuni hiyo imekwishasitisha uuzaji wa poda za watoto zenye ‘Talc’ duniani kote mwaka huu, baada ya kukabiliwa na maelfu ya kesi kutoka kwa wateja wakidai bidhaa za poda zenye ‘Talc’ zimesababisha Saratani kutokana na kuweka mazingira rafiki kwa visababishi vya ugonjwa huo.