Rushwa bandari ya Dar es Salaam

0
245

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Salum Hamduni amewasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan ripoti ya taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 iliyofanya uchambuzi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo bandari ya Dar es Salaam.

Amesema uchambuzi huo katika bandari ya Dar es Salaam umebaini maeneo ya utoaji huduma yenye vihatarishi vya rushwa ambayo ni pamoja ya forodha, ubebaji mizigo na mapato.

Hamduni amesema mifumo ya GePG, Cargo System na TANCIS, wateja kutojua taratibu na uwajibikaji hafifu kwa baadhi ya Watendaji wa bandari ya Dar es Salaam, ni miongoni mwa mambo yanayosababisha vihatarishi hivyo vya rushwa.