Tanzania yapongezwa kwa uwazi

0
239

Balozi wa Marekani nchini Dkt. Michael Battle ameipongeza Tanzania kwa uwazi na utoaji wa haraka wa taarifa kwa umma kuhusu ugonjwa wa Marburg ambao mpaka sasa umethibitishwa kusababisha vifo vya watu watano mkoani Kagera.

Dkt. Battle ametoa pongezi hizo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

“Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa wa wazi hasa katika utoaji wa taarifa za magonjwa ya mlipuko kwa haraka ikiwemo hii ya ugonjwa wa Murburg. Hakika mmeonyesha uongozi bora kwa dunia kuhusu usalama wa afya kwa Watanzania na dunia”. Amesema Balozi Battle.

Naye Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Tanzania itaendelea kutimiza wajibu wake kwa kuzingatia kanuni za Kimataifa za Afya kwa kutoa taarifa mapema ili kuweza kuwalinda Wananchi wake pamoja na usalama wa afya wa kimataifa.