Makazi kutathminiwa kwa drone

0
261

Wataalam wa uchukuaji picha za anga kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya ndege isiyo na rubani (drone), wameanza zoezi la majaribio la kuchukua picha za makazi katika mitaa mbalimbaali ya mkoa wa Dodoma.

Kupatikana kwa picha hizo kutasaidia kuonyesha hali halisi ya makazi na uendelezaji katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo ili kuruhusu shughuli ya upangaji na upimaji kufanyika.

Zoezi hilo linafanyika kama jaribio katika mtaa wa Bihawana jijini Dodoma, ambapo shughuli za urasimishaji zinatekelezwa kupitia mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi hapa nchini (LTIP).