Mlipuko waua 44 China

0
718

Idadi ya watu waliokufa baada ya kutokea mlipuko mkubwa katika kiwanda kimoja cha kutengeneza mbolea nchini China imefikia 44 na wengine 640 wamejeruhiwa.

Habari kutoka nchini China zinaeleza kuwa, mlipuko huo umesababisha kiwanda hicho cha Tianjiayi kilichopo kwenye  mji wa Yancheng kuwaka moto.

Idadi hiyo ya vifo inaifanya ajali hiyo  kuwa mbaya zaidi kati ya zote zilizowahi kutokea viwandani katika miaka ya hivi karibuni.Kati ya majeruhi 640 wanaopatiwa matibabu hospitalini, 32 hali zao ni mbaya na 58 wengine wamepata majeraha makubwa