Ligi mbalimbali dunia zimesimama kwa muda kupisha ratiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa ajili ya michezo ya timu za Taifa, ama za kimashindano au kirafiki.
Waksti Ligi Kuu ya NBC nchini Tanzania ikiendelea kufanya vizuri, idadi ya wachezaji kutoka kwenye ligi hii ambao wameitwa kwenye timu zao za Taifa inazidi kuongezeka.
Hii ni orodha ya mastaa walioitwa kwenye timu za Taifa pamoja na klabu ambazo wanatoka;
- Meddie Kagere (Rwanda), anatoka Singida BS
- Clatous Chama (Zambia), anatoka Simba SC
- Peter Banda (Malawi), anatoka Simba SC
- Pape Sakho (Senegal), anatoka Simba SC
- Henock Inonga (DR Congo), anatoka Simba SC
- Emmanuel Mvuyekure (Burundi), anatoka KMC
- Stive Nzigamasabo (Burundi), anatoka KMC
- Justin Ndikumana (Burundi), anatoka Coastal Union
- Fiston Mayele (DR Congo), anatoka Yanga SC
- Kennedy Musonda (Zambia), anatoka Yanga SC
- Kenneth Maguna (Kenya), anatoka Azam FC
- Khalid Aucho (Uganda), anatoka Yanga SC
- Stephane Aziz Ki (Burkina Faso), anatoka Yanga SC
- Saido Ntibazonkiza (Burundi), anatoka Simba SC