Mshambuliaji wa PSG na Ufaransa, Kylian Mbappe amethibitishwa kuwa nahodha wa timu ya Taifa, kocha mkuu Didier Deschamps ameeleza.
Mbappe mwenye miaka 24 ataongoza Les Bleus katika kuwania kufuzu fainali za Euro mwaka 2024, huku msaidizi wake akiwa Antoine Griezmann.
Kinda huyo ambaye aliibuka mfungaji bora wa Kombe la Dunia mwaka 2022, amechukua kitambaa hicho baada ya nahodha aliyekuwepo, Hugo Lloris kutundiga daluga kimataifa.
Septemba 2022 aliongoza timu hiyo katika mchezo dhidi ya Denmark na sasa anaweka rekodi ya kuwa nahodha mwenye umri mdogo zaidi kwenye timu hiyo. Jukumu lake la kwanza litakuwa Ijumaa wakati Ufaransa itakapokutana na Uholanzi.
Lloris ndiye nahodha aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi akiwa amevaa kitambaa cha unahodha tangu mwaka 2008 hadi mwaka 2022