Miwili ya Samia na TARURA Simiyu

0
306

Katika kipindi cha miaka miwili (2021-2023) Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) ilipokea jumla ya shilingi bilioni 25.08 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya barabara, madaraja na makalavati mkoani Simiyu.

Katika Bajeti ya mwaka 2021/2022, TARURA imepata ongezeko la fedha kutoka shilingi bilioni 5.88 mwaka 2020/2021 hadi billioni 18.10 sawa na ongezeko la asilimia 218%.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Gaston Pascal amesema barabara nzuri katika mkoa huo zimeongezeka kutoka kilomita 931 hadi kilomita 1,690.64, sawa na 40.64%, barabara zenye hali ya kuridhisha zimepungua kutoka kilomita 1,720 hadi kufikia kilomita 1,346.83, sawa na 32.34%.

Amesema madaraja yameongezeka kutoka 72 hadi kufikia 101, makalavati yameongezeka kutoka 423 hadi kufikia makalavati 912, taa za barabarani 131 zimefungwa katika wilaya za Itilima, Maswa, Bariadi na Meatu.