Rais Samia Suluhu Hassan amezipongeza timu za Simba na Yanga zote za mkoani Dar es Salaam kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa.
Rais Samia ametoa pongezi hizo mkoani Dar es Salaam wakati wa sherehe zilizoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) kwa lengo la kumpongeza kwa kutimiza miaka miwili madarakani.
“Kipekee niwapongeze sana Yanga na Simba kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye soka na niahidi kuwa nitaendelea kutoa motisha ya Milioni Tano kwa kila goli na pesa ipo kwa ajili yenu.” amesema Rais Samia
Pia amewapongeza Wadau wa michezo kwa kuendeleza michezo mbalimbali ukiwemo wa soka na kuahidi kutimiza ahadi ya Serikali ya kuendeleza sekta ya michezo.