Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) umeeleza kuridhishwa na kazi inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kuwatumikia Wananchi.
Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Mwenyekiti wa UWT Taifa Merry Chatanda wakati wa sherehe zilizoandaliwa na Umoja huo kwa lengo la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarakani.
Chatanda amesema kasi ya utendaji kazi ya Serikali ni ya kuridhisha na kazi inayofanywa ni nzuri ikiwa ni pamoja na usimamizi madhubuti wa miradi mbalimbali ya maendeleo.