Azzan : Askari trafiki walindwe

0
135

Mwenyekiti wa wenyeviti wa kamati za usalama barabarani nchini Idd Azzan ametoa wito kwa viongozi wa serikali na Jeshi la Polisi nchini kuwalinda askari wa usalama barabarani wanaosimamia sheria za uendeshaji wa vyombo vya moto.

Azzan pia amempongeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini kwa namna alivyochukua hatua dhidi ya kitendo alichofanyiwa askari wa usalama barabarani wakati akitimiza majukumu yake mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kufunga maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa mkoani Mwanza, Azzan amesema, askari wa usalama barabarani wanafanya kazi kubwa kudhibiti ajali, hivyo wanapaswa kulindwa na mamlaka zinazowasimamia.

Pia amewataka Wananchi kuheshimu sheria za barabarani ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika na hivyo kupunguza athari zitokanazo na ajali za mara kwa mara.