RC Malima : Serikali inaboresha maisha

0
141

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Adam Malima amesema, mabilioni ya fedha yanayotolewa na Serikali yanalenga kukuza uzalishaji na kuboresha maisha ya Wananchi wa mkoa huo.

Akizungumzia mafanikio ya mkoa wa Mwanza katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Malima amesema, Serikali imetoa fedha katika kila sekta na halmashauri ili kuboresha upatikanaji wa huduma kwa Wananchi wake.

Amesema kila mradi wa kimkakati na miradi ya kawaida Serikali imewekeza fedha nyingi, ili kuboresha maisha ya wananchi lakini pia kukuza uzalishaji na kuongeza kipato cha Wananchi.

Malima amesema, miradi ya maji, elimu, afya na miundombinu inawapa fursa Wananchi kukuza uchumi na kuongeza uzalishaji kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza.