MaDC watakiwa kuzingatia mipaka ya madaraka yao

0
255

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa wakuu wa wilaya nchini kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uzalendo na kujituma.

Dkt. Mpango ametoa wito huo jijini
Dodoma wakati akifungua mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa wilaya Tanzania Bara.

Pia amewataka
wazingatie mipaka ya madaraka yao na kuepuka migogoro na watendaji wengine hasa Wakurugenzi wa halmashauri.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango pia amesema kuna umuhimu kwa wakuu wilaya nchini kudhibiti siri za serikali.

Katika mafunzo hayo ya siku sita, mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa.